Gomes: Kwa kikosi hiki Wanasimba watafurahi sana

Pamoja na kupoteza mchezo kwa bao moja dhidi ya TP Mazembe katika kilele cha Simba Day, Kocha Didier Gomes ameridhishwa na viwango vya wachezaji wetu ambao asilimia kubwa ni vijana hasa wageni.

Gomes amesema wachezaji wanahitaji kupewa muda kuendelea kuzoeana ambapo anawaona wakiendelea kuwapa furaha Wanasimba ambayo wanaihitaji muda wote.

Akizungumzia mechi dhidi ya Mazembe, Gomes amesema mchezo ulikuwa na uwiano sawa na tulikuwa na nafasi ya kufunga kama ilivyokuwa kwao lakini wenzetu walikuwa imara kwenye ulinzi.

Gomes ameongeza kuwa ana matumaini makubwa na kikosi chetu na kuelekea kwenye mashindano mbalimbali tunaenda kufanya vizuri.

“Sikupenda matokeo ya mchezo lakini nimefurahishwa na viwango vya wachezaji. Wamecheza vizuri na tulikuwa na nafasi ya kupata mabao.

“Pia tungeweza kulizuia bao tulilofungwa lakini imeshatokea, ila kikosi changu kitaendelea kuimarika kadiri wachezaji watakavyokuwa pamoja na Wanasimba watafurahi,” amesema Gomes.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER