Chama, Che Malone, Kapombe wachuana mchezaji bora Septemba

Nyota wetu watatu wameingia fainali ya kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Septemba (Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao ni kiungo mshambuliaji, Clatous Chama na walinzi Che Fondoh Malone pamoja na Shomari Kapombe.

Katika mwezi Septemba tumecheza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Power Dynamos ugenini pamoja mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union.

Hizi ndio takwimu zao wote:

Dakika Magoli Assist

Chama 180 2 1

Che Malone 180 0 0

Kapombe 162 0 0

Zoezi la kupiga kura kupitia kwenye tovuti ya klabu ya www.simbasc.co.tz limeanza tayari na litafungwa Jumatano Oktoba 11 saa sita usiku.

Mshindi wa jumla atakayepata kura nyingi atapokea pesa taslimu Sh. 2,000,000 kutoka kwa Uongozi wa klabu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER