Bocco, Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi ya Yanga Leo

Nahodha John Bocco na Chris Mugalu wamepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wa Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga utakaopigwa saa 10 jioni katika Uwanja wa Lake Takanyika mjini Kigoma.

Kocha Didier Gomes ameona kuanza na wawili hao kutaongeza ufanisi kutokana na ukubwa na umuhimu wa mchezo wenyewe.

Bocco na Mugalu watapata msaada mkubwa kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Rally Bwalya na Luis Miquissone.

Katika kiungo wa ulinzi ataendelea kucheza Taddeo Lwanga huku Pascal Wawa na Joash Onyango wakisimama katika beki wa kati.

Aishi Manula ataendelea kusimama kwenye milingoti mitatu huku Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wakicheza pembeni.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Clatous Chama (17), Rally Bwalya (8), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Luis Miquissone (11).

Wachezaji wa Akiba – Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Mzamiru Yassin (19), Bernard Morrison (3), Medie Kagere (14), Hassan Dilunga (24).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER