Bocco, Manula, Zimbwe Jr kuchuana tuzo za IDFA leo

Nyota wetu watatu wanawania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwaka wa Klabu, zilizoandaliwa na Chama cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA).

Nyota waliongia fainali ya kinyang’anyiro hicho ni Nahodha John Bocco, mlinda mlango Aishi Manula na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Hafla ya tuzo hizo itafanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada uliopo Ilala jijini Dar es kuanzia saa 12 jioni.

Kura za kumpata mshindi zimepigwa na mashabiki kupitia namba iliyotolewa na IDFA wiki kadhaa zilizopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER