Bocco awataja mashabiki mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly

Nahodha wa timu, John Bocco amesema licha ya ugumu tutakaoupata kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly lakini uwepo wa mashabiki ambao watakuja kwa wingi uwanjani utatuongezea nguvu.

Bocco amesema mashabiki wana mchango mkubwa kuisaidia timu kupata ushindi nasi tutatumia nafasi hiyo kuhakikisha tunashinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri.

Bocco ameongeza kuwa haitakuwa mechi rahisi na kila mchezaji analijua hilo na maandalizi waliyopata anaamini tutapata ushindi.

“Haitakuwa mechi rahisi, Al Ahly ni timu bora lakini nasi tuna timu nzuri, tuna faida ya kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu ambao watakuwa wamezaja uwanja.”

“Kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo na tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya ili tuwe sehemu salama katika mechi ya marudiano,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER