Bocco awataja Kagere, Mugalu ufungaji bora VPL

Baada ya kufanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Msimu wa 2020/21 , Nahodha John Bocco amepongeza ushirikiano aliopata kutoka kwa washambuliaji wenzake Medie Kagere na Chris Mugalu.

Bocco amesema ulikuwa msimu bora kwao kama washambuliaji pamoja na wachezaji wote na kila aliyepata nafasi alifunga na ni moja ya chachu iliyosababisha ubingwa wa msimu huu.

Nahodha huyo ameongeza kuwa ushirikiano baina ya wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki umechangia mafanikio ya msimu huu.

“Kwa dhati niwapongeze washambuliaji wenzangu Kagere na Mugalu kwa ushirikiano walionipa hadi leo, ilikuwa aliye kwenye nafasi anapewa pasi na anafunga.

“Tulikuwa na msimu mzuri, ushirikiano ulikuwa mkubwa kuanzia wachezaji viongozi hadi mashabiki na hilo limechangia pakubwa kufanikisha hili,” amesema Bocco.

Bocco amemaliza akiwa kinara wa ufungaji kwa kutupia kambani mabao 16 akifuatiwa na Mugalu mwenye 15 huku Kagere akifunga 13.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER