Bocco awapiku Manula, Zimbwe Jr tuzo za IDFA

Nahodha John Bocco ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2020 wa Mashabiki zilizotolewa na Chama cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA).

Bocco amewashinda mlinda mlango Aishi Manula na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein Zimbwe Jr katika hafla ya tuzo hizo zilizofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.

Msimu wa mwaka 2020/21 ulikuwa bora kwa Nahodha Bocco kutokana na kushinda tuzo nyingi binafsi kama mfungaji bora wa ligi na mchezaji bora wa mwaka (MVP).

Katika hafla hiyo pia Klabu ya Simba imeshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka kutokana na mafanikio makubwa tuliyopata.

Msimu wa 2020/21 tulichukua mataji yote ya ndani Ligi Kuu, Azam Federation Cup, Ngao ya Jamii na kufika robo fainali ya michuno ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER