Beleke awaliza Ihefu dakika za majeruhi Highland Estate

Mabao mawili yaliyofungwa dakika saba kabla ya kumalizika mchezo yametosha kutupa ushindi wa 2-0 dhidi ya Ihefu FC katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa Uwanja wa Highland Estate.

Baleke ambaye amekuwa na urafiki mzuri na nyavu amefunga mabao matano katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Ihefu.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku wenyeji Ihefu wakitawala sehemu kubwa na kufika zaidi langoni kwetu lakini mashambulizi yao yaliishia mikononi mwa mlinda mlango, Ally Salim.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi ya haraka langoni kwa Ihefu lakini tulikosa umakini.

Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya 83 kwa shuti kali la mguu kushoto baada ya Pape Sakho kumtulizia ndani ya 18 kufuatia krosi ya Israel Patrick.

Baleke alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la pili dakika ya 86 kwa mpira wa tik tak akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kibu Denis.

Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 25 tukiendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

X1: Mapara, Wadada, Mbegu (Mwasapili 69′), Nyoso, Kisu, Onditi, Loth, Adam (Ngoah 62′), Mahundi, Chirwa, Yacouba.

Walionyeshwa kadi: Adam 46′ Mahundi 83′ Loth 83′.

X1: Ally, Israel, Gadiel, Kennedy, Onyango, Sawadogo (Kapama 21′), Sakho, Mzamiru, Baleke, Kyombo (Bocco 45′), Kibu

Walionyeshwa kadi: Gadiel 33′ Mzamiru 80′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER