Winga Peter Banda, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Banda amewapiku kiungo mshambuliaji, Pape Ousmane Sakho na mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe ambapo aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Banda raia wa Malawi atakabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.
Katika mwezi Machi Banda amecheza mechi nne sawa na dakika 226 akionyesha kiwango safi na kusaidia kupatikana kwa bao moja (assist).
Mchanganuo wa kura zilizopigwa kupitia tovuti ya klabu www.simbasc.co.tz
Banda kura 2,682 sawa na asilimia 74.
Sakho kura 744 sawa na asilimia 20.
Kapombe kura 218 sawa na asilimia sita.
One Response