Baleke Afungua akaunti tukipata pointi tatu Jamhuri

 

Bao pekee lililofungwa na mshambuliaji Jean Baleke limetosha kutupa ushindi dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Jamhuri.

Baleke alitupatia bao hilo dakika ya 47 kipindi cha kwanza akimalizia mpira wa kichwa uliopigwa Kibu Denis kufuatia mlinzi wa Dodoma na mlinda mlango kutegeana kuondoa hatari.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini zilikosa utulivu katika eneo la mwisho.

Kipindi cha pili tuliongeza mashambulizi huku wenyeji wakitumia dakika 15 za mwisho kutushambulia lakini safu yetu ya ulinzi ilikuwa imara.

X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Ouattara, Sawadogo (Kapama 71) Kibu, Erasto, Bocco (Kyombo 83), Baleke (Okrah 83) Ntibazonkiza

Walioonyeshwa kadi: Ntibazonkiza 18′ Kennedy 30′ Sawadogo 60′

X1: Mgore, Fadhil, Ngalema, Augustino, Justine, Nkosi, Mwana, Muhsin (Raizin 85), Opare (Karihe 85), Mwaterema, Martin (Zidane 63)

Walioonyeshwa kadi: Kibuta 32′ Justine 50′ Augustino 48′ Opare 57′ Karihe 89′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER