Kikosi chetu leo jioni kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Alhamisi saa moja usiku.
Baada ya sare ya jana dhidi ya watani Yanga wachezaji walipewa ruhusa ya kwenda kukutana na familia zao kabla ya kurejea mazoezini.
Mazoezi hayo ambayo yatafanyika katika Uwanja wa Mo Simba Arena yakimalizika kikosi kitaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo huo ambao tunajua utakuwa mgumu.
Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda katika kila mchezo ili kurejesha taji letu la ligi ambalo tulipoteza msimu uliopita.