Alichosema Robertinho baada ya ushindi dhidi ya Mtibwa

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi mara kwa mara ili wachezaji waendelee kuzoeana.

Robertinho amesema katika mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar alifanya mabadiliko machache ya wachezaji kipindi cha kwanza kabla ya kuwaweka wazoefu cha pili na kubadili mchezo.

Robertinho ameongeza kuwa tuliweza kucheza vizuri na kupata mabao mawili ya haraka kabla ya kupoteza umakini na kusababisha Mtibwa kusawazisha yote.

“Tunaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi taratibu ili wachezaji wazidi kuzoeana. Tuna timu bora lakini tunapaswa kucheza kitimu. Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu,” amesema Robertinho.

Akizungumzia makosa ya kiulinzi yaliosababisha Mtibwa kusawazisha mabao mawili, Robertinho amesema “unajua tunamkosa Henock Inonga ambaye ni mlinzi kiongozi.

“Henock alianza kuzoeana kiuchezaji na Che Fondoh Malone lakini ameumia. Tunae Kennedy Juma na Hussein Bakari wanafanya vizuri lakini wanapaswa kucheza pamoja mara kwa mara ili wawe bora zaidi,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER