Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kipigo cha mabao 5-1 tulichopata kutoka kwa watani Yanga ni sehemu ya mpira.
Robertinho amesema kipindi cha pili tulipoteza umakini na kushindwa kuzuia nafasi ambazo wapinzani wetu walizitumia vizuri.
Robertinho amesema hatukuwa vizuri wakati tunapopoteza mpira na wapinzani waliweza kutusoma na kutumia madhaifu yetu kuwa faida kwao.
“Nawapongeza wapinzani kwa ushindi hatukuwa vizuri hasa kipindi cha pili lakini huu ni mpira na tunajipanga kwa mchezo ujao,” amesema Robertinho.