Alichosema Mgosi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya JKT Queens

Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi amesema mchezo wa kesho wa fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya JKT Queens utakuwa mgumu lakini tutaingia uwanjani kwa nia ya kutaka kutwaa ubingwa.

Mgosi amesema JKT walitupokonya taji msimu uliopita kwa alama moja kwahiyo mchezo wa kesho utatoa picha kuelekea 2023/24.

Mgosi ameongeza kuwa kikosi cha Queens kipo tayari na tumefanikiwa kuwaona JKT walivyocheza mchezo uliopigwa dhidi ya Fountain Gate ambapo tumebaini ubora na mapungufu yao.

“Itakuwa mechi ngumu, JKT Queens ni mabingwa wa ligi msimu uliopita walituvua taji kwa tofauti ya alama moja nasi tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua ubingwa,” amesema Mgosi.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, mlinzi wa kati Vivian Corazone amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo huku akikiri haitakuwa mechi rahisi.

“Sisi kama wachezaji tumejiandaa kwa ajili mchezo huo, haitakuwa mechi rahisi lakini tupo tayari na lengo letu ni kuchukua taji,” amesema Corazone.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER