Alichosema Kocha Mgunda kuelekea mchezo wa kesho

Kocha wa muda Juma Mgunda, amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya saa 10 jioni.

Mgunda amesema baada ya kurudi kutoka Malawi timu imefanya mazoezi siku mbili jana na leo kabla ya kuanza safari kuelekea Mbeya.

Mgunda amewataja wachezaji wawili viungo wakabaji Victor Akpan na Sadio Kanoute kuwa hawatakuwa sehemu ya mchezo kwa sababu tofauti.

Akpan anaendelea kuuguza majeraha wakati Kanoute anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano hivyo kanuni haziruhusu kuwa sehemu ya mchezo wa kesho.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri, tumepata siku mbili za kufanya mazoezi jana na leo, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kupambana kuhakikisha tunarudi na pointi zote tatu,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER