Alichosema Kocha Mgunda kuelekea mchezo dhidi ya Coastal

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Mkwakwani yamekamilika.

Mgunda amesema tumesafiri na wachezaji 22 na wote wapo kwenye hali nzuri tayari kuipigania timu kupata alama tatu muhimu ugenini.

Mgunda ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na Coastal watapambana kuhakikisha tunashinda nyumbani lakini tumejiandaa kikamilifu kuwakabili.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, baada ya mechi yetu dhidi ya Polisi Tanzania kikosi kilirudi Dar es Salaam na siku iliyofuata tulianza mazoezi ya mchezo huu. Tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kikamilifu kupata ushindi,” amesema Mgunda.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema morali yao ipo juu na wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na benchi la ufundi kufanikisha malengo.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kuhakikisha tunapambana kufuata maelekezo ya walimu kwakuwa lengo letu ni kushinda,” amesema Salim.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER