Al Hilal watua jijini Dar

Mabingwa wa Soka nchini Sudan, Al Hilal wamewasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns kwa mwaliko maalumu wa klabu yetu.

Al Hilal wamepokelewa na Mratibu wa klabu Abbas Ally, Mhasibu Lucy Mngongo na Mkurugenzi wa Mashindano, Mzee Hamisi Kisiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na kuwafikisha katika Hoteli ya Holiday Inn iliyopo Posta walipofikia.

Baada ya kuwasili wachezaji wa Al Hilal watapumzika kwa saa chache kabla ya kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili kujiandaa na mchezo wa kesho wa kirafiki dhidi ya Namungo FC utakaopigwa saa moja usiku Uwanja wa Azam Complex.

Hilal watacheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Azam FC, Januari 31 katika Uwanja huo huo wa Azam Complex.

Miamba hiyo ya Sudan itaendelea na mazoezi ya maandalizi kabla ya kushuka katika dimba la Benjamin Mkapa Februari 5, kucheza nasi na utakuwa mchezo wa mwisho kabla ya kutimka kesho yake kuelekea Afrika Kusini kuifuata Mamelodi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER