Mlinda mlango, Aishi Manula amerejea langoni katika mchezo wa leo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni.
Aishi alifanyiwa upasuaji wa nyama za paja Mei, 30 mwaka huu nchini Afrika Kusini na leo ndio mechi yake ya kwanza ya ligi kurejea langoni.
Ukiacha Aishi kurejea langoni kuchukua nafasi ya Ally Salim kocha mkuu Robertinho Oliviera ‘Robertinho’ hafanya mabadiliko yoyote ya kikosi ukilinganisha na kile kilichocheza na Ihefu FC mchezo uliopita.
Kikosi Kamili kilivyopangwa:
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Henock Inonga (29), Che Malone (20), Fabrice Ngoma (6), Sadio Kanoute (8), Kibu Denis (38), Jean Baleke (4), Said Ntibazonkiza (10), Clatous Chama (17).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Jimmyson Mwanuke (21), Kennedy Juma (26), Hussein Kazi (16), Mzamiru Yassin (19), Luis Miquissone (11), Willy Onana (7), Moses Phiri (25), John Bocco (22)