Ahmed: Kambi ya Dubai ilikuwa ya mafanikio

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kambi ya siku ya nane tuliyofanya Mjini Dubai imekuwa na mafanikio kwa kuwa Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amepata muda wa kukaa pamoja na wachezaji.

Ahmed amesema baada ya Robertinho kukaa na wachezaji amewasoma tabia zao za ndani na nje ya uwanja hivyo itakuwa faida kwake kuwaongoza katika mechi za mashindano.

Kuhusu mechi mbili za kirafiki tulizocheza Ahmed amesema zilikuwa kipimo kizuri kwetu si tu kwa michuano ya ndani bali hadi Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itaendelea mwezi ujao.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumerejea salama jijini Dar es Salaam na kesho tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City kwenye Ligi Kuu ya NBC.

“Kambi yetu ilikuwa ya mafanikio mjini Dubai Kocha Robertinho amepata nafasi ya kukaa na wachezaji pia tumepata mechi nzuri za kirafiki ambazo zimetuonyesha mahali kikosi chetu kilipo kuelekea michuano iliyo mbele yetu,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER