Ahmed amkabidhi Rais Karia ‘Uzi’ wa kuivaa dhidi ya Al Ahly

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amemkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia jezi rasmi ambayo ataivaa katika mchezo wetu wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Machi 29 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Rais Karia aliweka hadharani kuwa atavaa jezi ya timu inayocheza michuano ya kimataifa na atahudhuria uwanjani ikiwa ni sehemu ya kutoa mchango wake.

Baada ya kutoa kauli hiyo Menejimenti ya klabu ikaona ni jambo jema kumpatia jezi maalum ambayo ataivaa siku ya mchezo.

Simba inafarijika kuona kiongozi wa juu katika Mamlaka ya mpira nchini kujitoa kwa ajili ya kuhamasisha watu waziunge mkono timu zao za nyumbani huku akionyesha mfano.

Tumempa jezi namba 11 ikiwa ni kumbukumbu nzuri ya vipaumbele vyake 11 alivyovitoa wakati akigombea Urais wa TFF kwa mara ya kwanza mwaka 2017

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER