Ahmed aelezea utaratibu mzima mchezo dhidi ya Raja Casablanca

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema baada ya kikosi kuwasili kutoka Guinea alfajiri ya leo wachezaji wameingia kambini moja kwa moja kuajindaa na mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigiwa Jumamosi, Benjamin Mkapa.

Ahmed amesema matokeo ya mchezo uliopita dhidi Horoya yametupa somo na yametufanya kuongeza makini ili kuhakikisha haturudii makosa.

Ahmed ameongeza kuwa tunajua mpira una matokeo matatu lakini sisi Jumamosi tunahitaji ushindi pekee dhidi ya Raja.

Ahmed pia ametolea ufafanuzi kuhusu masuala yafuatayo:

MUDA WA MCHEZO

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetaka mchezo ufanyike saa moja usiku, awali tulivyothibitisha tarehe ya mchezo tulitaka mechi iwe saa 10 jioni.

WAAMUZI KUTUA KESHO

Waamuzi wa mchezo watatoka nchini Cameroon na wanatajia kuwasili kesho huku Maafisa wengine wakiendelea kuwasili ndani ya siku mbili hizi.

RAJA HAIJATHIBITISHA INATUA LINI

Tumewasiliana na Raja Casablanca ili kujua wanawasili lini tuwaandalie mahali pa kufikia pamoja na maandalizi ya mchezo lakini bado hawajibu chochote mpaka sasa.

NTIBAZONKIZA YUPO TAYARI KWA RAJA

Kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza ambaye aliukosa mchezo uliopita dhidi ya Horoya kutokana na majeruhi amepona na sasa yupo kambini na wenzake kujiandaa na mchezo wa jana.

KANOUTE KUIKOSA RAJA

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute ataukosa mchezo wa Jumamosi kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

WACHEZAJI WAFURAHIA AHADI YA RAIS SAMIA

Ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi ya kununua kila bao tutakalofunga kwa Sh. 5,000,000.

Wachezaji wamefurahi na wamelichukua kama agizo la Rais na wameahidi kupambana kuhakikisha tunafunga mabao mengi kwa kadri tutakavyoweza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER