Manula: Tunazidi kukua katika Soka la Afrika

Mlinda mlango namba moja, Aishi Manula amefunguka kuwa kadiri muda unavyozidi kwenda tunaendelea kupata uzoefu wa kupambana na miamba ya soka barani Afrika kutokana na kushiriki michuano hiyo mara kwa mara.

Manula amesema kila mwaka tunapanda viwango vya uchezaji kitu ambacho anaamini baada ya miaka michache ijayo tutatikisa Bara la Afrika.

Manula ameongeza kuwa changamoto tunazopata katika michuano ya Afrika zinazidi kutujenga na kutuimarisha ambapo msimu ujao tutakuwa bora zaidi ya ilivyo sasa.

“Mimi ninaamini tunazidi kukua siku hadi siku. Tumefika robo fainali mara nne lakini safari hii tumetolewa kwa penati. Msimu ujao tutakuwa bora zaidi. Tumeimarika na changamoto za Afrika tunazijua,” amesema Manula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER