Leo saa 2:15 usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa New Amaan Complex kuikabili Singida Fountain Gate katika mchezo wa pili wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha amefanya mabadiliko ya wachezaji sita ukilinganisha na wale walioanza kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKU.
Benchikha amewaanzisha Ally Salim, Israel Patrick, Kennedy Juma, Abdallah Khamis, John Bocco na Willy Onana kuchukua nafasi za Ayoub Lakred, David Kameta, Hussein Kazi, Jimmyson Mwanuke, Shaban Chilunda na Luis Miqussone,
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Che Malone (20), Abdallah Hamisi (13), Moses Phiri (25), Sadio Kanoute (8), John Bocco (22), Fabrice Ngoma (6), Willy Onana (7).
Wachezaji wa Akiba:
Ahmed Teru (31), David Kameta (3), Hussein Kazi (16), Jimmyson Mwanuke (21), Luis Miquissone (11), Salem Karabaka (23), Mohamed Mussa (14), Shaban Chilunda (27), Jean Baleke (4).