Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena kujiandaa na Dodoma

Kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji.

Morali ya wachezaji ipo juu na wapo tayari kuhakikisha wanapambana kwa dakika zote 90 ili ushindi upatikane.

Wachezaji wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna aliyepata maumivu yoyote ambayo yanaweza kumfanya kukosa mchezo.

Mchezo huo ambao utakuwa wa pili wa Ligi Kuu kwetu utapigwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam saa 10 jioni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER