Rasmi Uwanja Umejaa

Zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kilele cha Simba Day tiketi zote 60,000 zinazojaza Uwanja wa Benjamin Mkapa zimeuzwa (Sold Out).

Hii ni mara ya kwanza kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kujaa siku tatu kabla ya tukio nasisi ndio tumeweka historia.

Tiketi za Platnum ziliisha siku moja baada ya kutangazwa kuuzwa zikifuatiwa na VIP A siku mbili baadae.

Mageti ya uwanja yatafunguliwa mapema saa 2 asubuhi siku Jumapili ili mashabiki walionunua tiketi waingie mapema na kuondoa usumbufu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER