Taarifa kwa Umma

Klabu yetu imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi Zoran Maki.

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mikataba ya Kocha wa viungo Sbai Karim na Kocha wa makipa Mohammed Rachid.

Uongozi wa klabu ya Simba unawashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila heri katika majukumu yao mapya.

Kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya KMC kikosi chetu kitakua chini ya Kocha msaidizi Selemani Matola.

Tayari mchakato wa haraka wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Simba Nguvu Moja.

Barbara Gonzalez
Afisa Mtendaji Mkuu
Simba Sports Club
06 Sept, 2022

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER