Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mussa Azan Zungu ndiye mgeni rasmi wa mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Jumapili saa 10 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mh. Zungu ni mwanachama wetu na amekuwa akishiriki matukio mbalimbali ya klabu kama mikutano kila anapopata nafasi.
Mh. Zungu amechaguliwa leo kuwa Naibu Spika akijaza nafasi iliyoachwa na Dk. Tulia Akson ambaye amekuwa Spika na atatuongoza Wanasimba Jumapili dhidi ya ASEC uwanjani.