Zoran: Tupo tayari kwa Derby kesho

Kocha Mkuu Zoran Maki, ameweka wazi kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya NBC.

Zoran amesema tunajua mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa ni Derby lakini tumewaandaa wachezaji wetu kuhakikisha tunapata ushindi.

Ingawa ndiyo mchezo wake wa kwanza wa Derby Kocha Zoran amesema hana presha kwa kuwa amecheza derby nyingi ndani ya Afrika na kule Saudi Arabia.

“Tupo tayari kwa mchezo, tunajua mchezo utakuwa mgumu. Hakuna mchezo wa Derby ambao ni rahisi lakini tupo tayari kushindana na kushinda.

“Binafsi sina presha na kesho haitakuwa Derby yangu ya kwanza, nimecheza Derby Morocco, Sudan Algeria na Saudia Arabia kwahiyo haitakuwa na tofauti,” amesema Zoran.

Kwa upande wake Nahodha John Bocco amesema wachezaji wapo tayari kwa mchezo wamepata maandalizi mazuri kutoka kwa makocha na tutahawaheshimu wapinzani lakini tumejiandaa kushinda.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, lakini tumepata maandalizi mazuri, wachezaji wapya wanaendelea kuzoea mazingira na wanafanya vizuri. Lengo letu ni kuwapa furaha mashabiki kwa kushinda kesho,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER