Zoran: Tuna kazi ya kufanya kabla ya kuanza ligi

Kocha Mkuu Zoran Maki, ameweka wazi kuwa tunahitaji kufanya marekebisho ya kiuchezaji kabla ya kuanza Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2022/23.

Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambapo amesema tunahitaji kufanya jitihada ili kuanza vizuri msimu.

Zoran amesema katika mchezo wa jana tulikuwa bora zaidi kipindi cha kwanza kabla ya wenzetu kurudi cha pili nasi kufanya makosa yaliyosababisha kupoteza mechi kitu ambacho hatupaswi kufanya kwenye ligi.

“Tunahitaji kufanya marekebisho ya kiuchezaji kuelekea msimu mpya wa ligi. Kuna mapungufu yalitokea jana tunahitaji kurekebisha,” amesema Kocha Zoran.

Mchezo wetu wa kwanza wa ligi utakuwa dhidi ya Geita Gold, Alhamisi Agosti, 18 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER