Zoezi la kubandika picha za hamasa kuelekea ufunguzi wa African Football League limeanza rasmi Magomeni Mikumi katika Tawi la Mpira Pesa.
Zoezi hilo limeongozwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally ambaye alikuwa akigawa stika mwenyewe.
Makundi mbalimbali yakiwemo madereva bodaboda na bajaji wamevipamba vyombo vyao kwa stika za AFL.
Baada ya kumaliza Magomeni Mikumi kikosi kimeelekea Manzese na kunyoosha moja kwa moja hadi Mbezi Stendi ya Magufuli.