Zoezi la hamasa lahitimishwa Mbagala

Zoezi la kuhamasisha mashabiki kuelekea mchezo wetu wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto limehitimishwa leo katika viwanja vya Mbagala Zakhem.

Zoezi hilo lilianzia Magomeni kupitia Karume hadi Mbagala ambapo mashabiki wameendelea kununua tiketi za mchezo pamoja na jezi.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema ameridhishwa na mwitikio wa Wanasimba wanaojitokeza kwa wingi kila tunapopita hatua inayotufanya tuamini watajitokeza wengi uwanjani.

“Mwitikio umekuwa mzuri kuanzia jana hadi leo Wanasimba mmejitokeza kwa wingi, zoezi la kuhamasisha limeisha kilichobaki ni kujitokeza kwa wingi kesho kuja kuwapa sapoti wachezaji.

“Ni kweli tumepata ushindi ugenini lakini bado hatujafuzu, wingi wetu uwanjani utawafanya wachezaji kujiona wana deni kubwa na kupambana mwanzo mwisho kwa ajili ya furaha yetu,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER