Zimebaki pointi mbili tu tukae ‘mahala petu’

Ushindi wa bao moja tuliopata dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa CCM Kambarage umetufanya kubakisha alama mbili kabla ya kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Moja ya sababu iliyosababisha kupata ushindi huu mdogo ni kutokana na mazingira ya uwanja kutokuwa rafiki huku nyasi zikiwa ndefu na kupelekea kushindwa kucheza soka letu tuliolizoea.

Tulianza mchezo huo kwa kasi kwa kuliandama lango la Mwadui lakini hata hivyo hatukuweza kuzitumia nafasi tulizotengeneza kipindi cha kwanza huku mashambulizi mengine yakiishia kwa walinzi wa Mwadui.

Nahodha John Bocco alitupatia bao letu pekee kwa kichwa dakika ya 66 akimalizia mpira uliounganishwa kwa kichwa pia na mlinzi Joash Onyango kufuatia kona iliyopigwa na Bernard Morrison.

Kocha Didier Gomez aliwatoa Jonas Mkude, Perfect Chikwende na Rally Bwalya kuwaingiza Morrison, Bocco pamoja na Mzamiru Yassin.

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 52 tukipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo huku tukiwa na michezo mitatu mkononi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER