ZIMEBAKI NNE TU TUKAE TUNAPO STAHILI

Ushindi wa mabao 3-0 tuliopata kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya JKT Tanzania umetufanya kufikisha alama 45 ambazo ni nne pungufu ya wanaongoza.

Mchezo wa leo ni wa 19 huku tukiwa na mechi mbili mkononi dhidi ya vinara na endapo tutashinda viporo vyetu tutakuwa juu kwa tofauti ya alama mbili.

Mshambuliaji Chris Mugalu alitufungia bao la kwanza dakika ya nane kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Luis Miquissone aliyemuhadaa mlinzi mmoja wa JKT.

Miquissone alitufanya twende mapumziko tukiwa mbele kwa mabao mawili baada ya kuongeza jingine dakika ya 37 akimalizia pasi iliyopigwa na Erasto Nyoni.

Mlinda mlango wetu Aishi Manula alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kugongana na mshambuliaji wa JKT, Danny Lyanga dakika ya 65.

Nahodha John Bocco aliyeingia kipindi cha pili alikamilisha karamu ya mabao baada kufunga la tatu dakika za nyongeza akimalizia pasi ya Rally Bwalya.

Kocha Didier Gomez aliwatoa Miquissone, Mugalu na Aishi na kuwaingiza Bwalya, Bocco pamoja na mlinda mlango Aishi Manula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER