Nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema kambi ya Misri ilikuwa bora na wamepata maandalizi mazuri.
Zimbwe Jr ameyasema hayo muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere alitokea nchini Misri tulipokuwa tumeweka kambi ya wiki tatu.
Mlinzi huyo wa kushoto ameongeza kuwa kambi ilikuwa tulivu na wamepata kila kitu walichohitaji kilichobaki ni kwenda kukionyesha kwa vitendo uwanjani.
“Kambi ilikuwa nzuri, tunamshukuru Mungu tumerejea nchini salama tukiwa na nguvu ya kuwaonyesha Wanasimba kile tulichokifuata Misri,” amesema Zimbwe Jr.
Akizungumzia kuhusu nyota wapya waliosajiliwa msimu huu Zimbwe amesema “ni wachezaji wazuri wameonyesha wana kitu kikubwa watakiongeza kwenye timu ila sisi wakongwe huwa tunawaelekeza mipango na kinachohitajika kwa sasa.”