Zimbwe Jr: Ni mechi ya hatma kwetu

Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema mchezo wa kesho dhidi ya watani Yanga utaamua hatma yetu ya ubingwa ndio maana tumeupa umuhimu mkubwa.

Zimbwe Jr amesema endapo tutapata ushindi tutawasogelea wapinzani na tukipoteza tutajiweka mbali au kuupoteza ubingwa.

Zimbwe Jr ameongeza kuwa maandalizi ya mchezo yameenda vizuri, wamepokea mafunzo waliyopewa na walimu na wapo tayari kuyafuata.

“Tunajua ukubwa na umuhimu wa mechi ya kesho, tunajua wakitufunga wanatuacha mbali na tukiwafunga tunapunguza alama.

“Mechi ya kesho inaamua hatma yetu ya ubingwa msimu huu, nikuhakikishie tumejipanga kupata matokeo chanya.

“Kitu ambacho kinatufanya kupambana kupata alama tatu kwanza ni kulisogelea taji la Ligi, pamoja na kuhakikisha Yanga haitufanyi daraja la wao kuchukua ubingwa,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER