Nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ana matumaini makubwa ya kuiona timu yetu ya Simba ikinyakua ubingwa wa Ligi Kuu Msimu huu wa 2020/21 kwa mara ya nne mfululizo.
Zimbwe Jr ametoa kauli hiyo akisistiza inatokana na uwezo wa wachezaji waliopo kwenye kikosi chetu, benchi la ufundi na uongozi kuwajibika ipasavyo.
Mlinzi huyo wa pembeni ameongeza kuwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Polisi Tanzania utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda ili kuendana na matarajio yetu ya kutwaa taji hilo.
“Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza tuliwafunga lakini haimaanishi itakuwa rahisi kwao kutufunga Jumamosi. Tumejipanga kuondoka na alama zote tatu.
“Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu, Polisi Tanzania ni timu nzuri lakini sisi ni bora zaidi yao na malengo yetu ni kutetea ubingwa hivyo tumejipanga kushinda,” amesema ‘Zimbwe Jr’.
One Response
As a Simba fan , am really happy on how the team is developing on and off the pitch. The CEO an the whole Management is driving the club forward. When should we expect on the issuance of IPO