Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho kwa ajili ya kutupa sapoti kwenye mchezo wetu wa hatua ya pili ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Eagle FC.
Zimbwe amesema hamasa za mashabiki uwanjani zinasaidia wachezaji kupambana kuhakikisha ushindi unapatikana.
Akizungumzia mchezo wenyewe Zimbwe amesema anaamini utakuwa mgumu wenye ushindani lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunashinda na kuvuka hatua inayofuata.
“Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho waje watupe sapoti tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu hata kama ipo daraja la chini,” amesema Zimbwe Jr.