Zimbwe Jr awaita mashabiki kusherekea ubingwa kwa Mkapa Jumapili

Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amewataka mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi katika mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Namungo FC ambao tutakabidhiwa taji letu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Msimu wa 2020/21.

Zimbwe Jr amesema itapendeza kama mashabiki wataujaza uwanja wa Benjamin Mkapa kwa rangi nyekundu na nyeupe ili kuzipendezesha shamra shamra za ubingwa.

Mlinzi huyo wa kushoto amesema tutahakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huo kwa sababu haitapendeza kukabidhiwa ubingwa huku tukiwa tumefungwa au kupata sare.

“Tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi Jumapili, tunataka uwanja upambwe kwa rangi nyekundu na nyeupe ili shamra shamra za ubingwa zifane.

“Mashabiki waje tu uwanjani tuna imani tutawafurahisha kwa kupata ushindi. Tumejipanga vizuri kuhakikisha sherehe za ubingwa zinanogeshwa na ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

Aidha mlinzi huyo ameongeza kuwa kama wachezaji wamejipanga kuhakikisha tunachukua ubingwa tena msimu ujao ambao utakuwa ni mara ya tano mfululizo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER