Zimbwe Jr awaita mashabiki kuimaliza Ihefu Kesho

Nahodha Msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amewaomba mashabiki kujitojeza kwa wingi kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu FC utakaopigwa Uwanja wa Highland Estate, Ubaruku Mbarali saa 10 jioni.

Zimbwe Jr amesema mashabiki wana mchango mkubwa huku akiwaahidi furaha baada ya dakika 90.

Zimbwe ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu sababu tumetoka kuwafunga Ihefu kwenye michuano ya Azam Sports Federation siku mbili zilizopita hivyo watataka kulipa kisasi.

“Haitakuwa mechi rahisi Ihefu ni timu nzuri na jambo jingine litakalofanya mchezo kuwa mgumu ni kutokana tumetoka kuwafunga juzi kwahiyo na wao watataka kulipa kisasi.

“Kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutupa sapoti, sisi wachezaji tupo kamili kuhakikisha pointi tatu zinapatikana,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER