Zimbwe Jr afunguka ushindi dhidi ya Coastal

Nahodha msaizidi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema ushindi wa mabao 2-1 tuliopata dhidi ya Coastal Union ulikuwa muhimu kwetu kwa kuwa tunataka kupunguza idadi ya pointi tulizoachwa na vinara.

Zimbwe Jr amesema lengo letu ni kutetea ubingwa wa ligi hivyo kila mchezo kwetu ni fainali ili kuwafikia wanaongoza.

Mlinzi huyo wa kushoto ameongeza kuwa ushindi tuliopata leo umeonyesha kuwa sisi ni timu kubwa na tunaweza kufanya lolote wakati wowote.

Hata hivyo Zimbwe Jr amekiri mchezo ulikuwa mgumu na Coastal walijitahidi kutumia vizuri uwanja wao nyumbani lakini hata hivyo tulikuwa bora zaidi yao.

“Huu ushindi ni muhimu kwetu, idadi ya pointi tulizoachwa na vinara ni kubwa. Hatupaswi kuangusha tena alama kwa kuwa bado lengo letu ni kutetea ubingwa,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER