Zimbwe amaliza utata, asaini miwili

Baada ya maneno mengi yaliyozua mjadala katika mitandao ya kijamii, hatimaye Nahodha Msaidizi Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amemaliza utata baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kubaki kikosini.

Kwa takribani wiki moja sasa kumekuwa na taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kwamba nyota huyo atatimka baada ya kumaliza mkataba wake lakini kutokana na uwezo wake uongozi umeamua kumpa kandarasi mpya.

Kwa maana hiyo mfungaji huyo wa bao pekee katika mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Gwambina FC ataendelea kuvaa jezi nyekundu na nyeupe hadi mwaka 2023.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER