Yusuph Kagoma ni Mnyama

Kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma ni mchezaji wetu mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu ya kukitumikia kikosi chetu kutoka Singida Fountain Gate.

Kagoma ni moja ya vijana wazawa wenye uwezo mkubwa wa kuzuia timu ikishambuliwa na kupandisha mashambulizi.

Uwezo wake na umri wake ni miongoni mwa vigezo vilivyotuvutia kutafuta saini yake na tuna matarajio makubwa kutoka kwake.

Kagoma yupo kwenye mipango ya maboresho makubwa ya kuirejesha timu katika ubora ambao mashabiki wetu wanatamani kuiona.

Malengo ya Uongozi ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi imara kitakachokuwa na uwezo wa kuturejeshea mataji makubwa ambao tumeyapoteza katika miaka ya karibuni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER