Yussif Basigi Kocha mpya Simba Queens

Timu yetu ya Simba Queens kuanzia sasa itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Yussif Basigi ambaye anachukua nafasi iliyoachwa na Juma Mgunda aliyemaliza mkataba wake.

Basigi raia wa Ghana mwenye umri wa maiaka 52 tayari yupo nchini akiendelea kukisuka kikosi cha Queens.

Basigi anatarajiwa kuanza kuonekana katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.

Basigi ambaye amejiunga nasi akitokea Hasaacas Ladies ya nchini kwao Ghana.

Mwaka 2015 alipata medali ya dhahabu akiwa kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Ghana (Black Queens) ambaye aliiongoza kwenye michuano ya All African Games.

Mwaka 2021 Basigi aliiwezesha Hasaacas Ladies kumaliza nafasi ya tatu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake.

Kocha Mussa Mgosi ataendelea kubaki kuwa Msaidizi wa Basigi kama ilivyokuwa kwa Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER