Klabu yetu imemuuza kiungo mshambuliaji wake Andre Willy Esomba Onana kwenda klabu ya Al Hilal Benghazi ya Libya.
Onana alijunga nasi msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili na baada ya kuutumikia mwaka mmoja lakini sasa amepata malisho sehemu nyingine na ni rasmi amejiunga na Benghaz.
Onana alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kufunga magoli mawili kwenye mechi ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi Wydad Casablanca katika Uwanja wa Benjamini Mkapa msimu uliopita.
Simba inathamini mchango wa Onana kwa muda wote wa mwaka mmoja aliyodumu nasi.
Uongozi wa klabu ya Simba unamtakia kila la heri Onana katika maisha yake mapya ya soka.