Wiki ya Simba ‘Unyama Mwingi’ kuzinduliwa Buza Agosti Mosi

Ni rasmi wiki ya Simba ambayo imepewa jina la ‘Unyama Mwingi’ itaanza Jumamosi Julai 29 ambapo shughuli mbalimbali za kijamii zitafanyika kama tunavyofanya tangu tulipoanza Tamasha hili.

Wiki ya Simba itaanza Julai 29 lakini itazinduliwa rasmi Agosti Mosi katika Viwanja vya Buza Kanisani ambao Wanasimba wote tutakuna hapo.

Vikundi mbalimbali vya hamasa vitakuwepo kuhakikisha burudani inakuwa ya kutosha ambapo jezi mpya za msimu pamoja na tiketi za Simba Day zitapatikana.

Miongoni mwa matukio ambayo yatafanyika katika Wiki ya Simba ni kutembelea mashujaa pamoja na wazee wa klabu ili kutambua na kuthamini mchango wao kwa klabu kwenye nyakati zao.

Pia Uongozi wa klabu umesisitiza kwa Viongozi wa matawi kuhakikisha wanafanya marekebisho katika Ofisi zao kama kupaka rangi, kubadili bendera zilizokaa muda mrefu ili kuwa na muonekano mzuri nchini nzima.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER