Wawa naye kuagwa kwa Mkapa kesho

Mlinzi wa Kimataifa kutoka Ivory Coast, Pascal Wawa ataagwa rasmi kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya miaka minne ya kutumikia kikosi chetu.

Tutautumia mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kumuaga mlinzi huyo ili kuonyesha thamani na mchango wake mkubwa kwa muda wote aliodumu nasi.

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema mbali na kuagwa kwa mlinzi huyo kutakuwa na tukio la kuuaga mashabiki kwa kuwa mchezo wa kesho ni wa mwisho wa nyumbani msimu huu.

Ahmed ameongeza kuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez atatembelea vikundi vyote vya hamasa uwanjani ili kuwashukuru kwa kujitoa kwa ajili ya timu msimu mzima.

“Kama tulivyotangaza jana, tutautumia mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa kumuaga mlinzi wetu Pascal Wawa ambaye amedumu nasi kwa miaka mitano na amechangia pakubwa mafanikio tuliyopata.

“Tukio jingine litakuwa viongozi kuaga mashabiki kutokana na kutokata tamaa kuendelea kuipigania timu na Mtendaji wetu mkuu, Barbara atazunguka uwanja mzima kusalimia vikundi vya hamasa,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER