Mlinzi wa kati Pascal Wawa ataongoza idara ya ulinzi katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa leo saa moja usiku.
Katika siku za karibuni Wawa amekuwa akianzia benchi na kuingia kipindi cha pili lakini leo Kocha Pablo Franco ameamua kumpa nafasi ya kuanza.
Wawa atacheza sambamba na Joash Onyango katika beki wa kati kama ilivyokuwa msimu uliopita kabla ya Henock Inonga kuingia kikosini.
Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji na atapata msaada wa karibu kutoka kwa Clatous Chama, Pape Sakho na Peter Banda.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Erasto Nyoni (18), Peter Banda (11), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Clatous Chama (17), Pape Sakho (10)
Wachezaji wa Akiba
Aishi Manula (28), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Taddeo Lwanga (4), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38), Jimmyson Mwanuke (21)
One Response