Watatu waitwa Stars kujiandaa na Uganda

Wachezaji wetu watatu wameitwa kwenye Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi mbili za kufuzu Fainali za Afrika (AFCON) dhidi ya Uganda ‘The Cranes’.

Wachezaji walioitwa ni walinda mlango, Aishi Manula na Beno Kakolanya pamoja na kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin.

Baada ya mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya utakaopigwa Jumamosi nyota hao wataruhisiwa kwenda kujiunga na Taifa Stars.

Mechi hizo mbili za nyumbani na ugenini zitapigwa ndani ya mwezi huu ambapo ya kwanza itakuwa Machi 24 na ile ya marudiano itakuwa Machi 28.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER