Watatu kuchuana tuzo ya mchezaji bora mwezi Aprili

Nyota watatu wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao waliongia kwenye kinyang’anyiro hicho ni Clatous Chama, Aishi Manula na Shomari Kapombe ambao mmoja wao atashinda kutokana na idadi ya kura atakazopata.

Wachezaji watano waliingia kwenye kinyang’anyiro hicho lakini Kamati maalumu iliwachuja na kubaki na watatu ambao watapigiwa kura na mashabiki kupitia Tovuti rasmi ya klabu. Nyota wawili ambao walifika hatua hiyo ni Luis Miquissone na Pascal Wawa.

Tuzo hii ambayo inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile itakuwa ni ya tatu kutolewa tangu ilipoanza mwezi Februari mwaka huu.

Mchezaji atakayepata kura nyingi atakabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium.

Miquissone alikuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mwezi Februari wakati Joash Onyango alishinda mwezi Machi.

PIGA KURA YAKO HAPA CHINI

This poll has ended (since 3 years).
Clatous Chama
50.48%
Aishi Manula
30.74%
Shomari Kapombe
18.78%
SHARE :
Facebook
Twitter

138 Responses

  1. Kiuhalisia mchezaji bora wa mwezi wa nne kwa upande wa Simba ni Aishi manula, japo Chama atapewa kwa sababu ya jina lake (fanbase) Manula anasitahiri tuzo hii absolutely

  2. kapombe bwana anafaa kupata tuzo yake tusamini mchango wake
    Wote wapo vizuli lakin mwezi huu tumasain na yeye

    1. Sio bahati mbaya chama kuchukua he deserve to take it if you look on his contribution first he scored goals and he gave many goal assists

  3. Binafsi Nampa nafasi clatous chota chama kuwa mchezaji Bora wa mashabiki kwa mwezi April kutokana na kuhusika moja kwa moja kwenye magoli 20 yaliyofungwa na club ya Simba kwenye ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2020/21

  4. Binafsi tuzo itue kwa CHAMA kwa sababu kwenye hizi game za hapa karibuni kwa % kubwa amechangia upatikanaji wa ushindi kwa mnyma simba

  5. Aishi Salum Manula anastahili kabisa kutwaa tuzo hii maana amejitahidi sana kulinda lango na kutoruhusu magoli ya kizembe!! #Manula

  6. Kumpa Aishi Manula ni chachu ya kumfanya awe bora zaidi langoni tusiangalie wachezaji wa ndani ya uwanja hata wa golini pia tuwathamini

  7. Air Manula Tz one anafaa sana kupata tuzo bt Triple C nae hapoi kabisa..
    #Nguvumoja
    🦁💪🔥✈️🙏🇹🇿

  8. Dah Manula alistahili sana kipindi ichi @Hongeara Chama Jr

  9. Hii tuzo anayestahili kuichukua ni Aishi Salum Manula, ila Chama ana jina kubwa ndio maana atashinda yeye.

  10. Kura yangu nampa kapombeeeee hawampi lakin kaka uyu yuko vizuri sana asa wakati wa kupandisha na kumwaga majaro na V pass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER