Watano kupaa leo kuungana na wenzao Misri

Nyota wetu watano ambao walibaki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu leo mchana watasafiri kuelekea Misri tayari kujiunga na wenzao kwenye maandalizi ya kuanza msimu mpya wa ligi.

Juzi kikosi cha wachezaji 19 pamoja na benchi la ufundi kilitangulia Misri huku wengine wakibaki kukamilisha baadhi ya taratibu ikiwemo suala la visa.

Nyota hao ambao wataondoka leo ni mshambuliaji Moses Phiri, viungo Nassor Kapama, Taddeo Lwanga, Peter Banda na mlinzi Henock Inonga.

Wachezaji wengine watano ambao wapo kwenye kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na michuano ya CHAN wao watasubiri mpaka wamalize majukumu yao.

Kikosi chetu kitakuwa nchini Misri kwa takribani wiki tatu kabla ya kurejea nchini tayari kwa kuanza msimu mpya wa ligi 2022/23.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER